Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters gazeti hilo sasa litakuwa likiakisi matukio hayo kwa kiwango cha chini. Kwa mujibu wa Abdul Hussein Sultan mhariri mkuu wa gazeti hilo la ad-Dar, gazeti hilo sasa halitakuwa likiakisi matukio ya nchi zilizotajwa kwa kina bali litakuwa likiakisi tu ripoti zitakazokuwa zikitolewa na mashirika ya kutetea haki za binadamu kama vile Amnesty International na Human Rights Watch. Zaidi ya thuluthi moja ya raia milioni moja na laki moja wa Kuwait ni Mashia na wana nafasi muhimu katika Wizara za Biashara na Vyombo vya Habari za Kuwait. Licha ya Kuwa Mashia wana uhuru nchini humo ikilinganishwa na nchi nyingine za Kiarabu lakini bado serikali huwakandamiza na kufunga magazeti yao kwa visingizio visivyo na msingi. 1013219