IQNA

Msikiti mrefu zaidi duniani kujengwa Algeria

11:44 - May 24, 2012
Habari ID: 2332993
Wafanyakazi wameanza kuweka misingi wa msikiti utakaokuwa mrefu zaidi duniani pamoja na msikiti wa tatu kwa ukubwa duniani.
Kwa mujibu wa tovuti ya Islam Today, mradi huo utakaoghrimu Euro bilioni moja utajumuisha mnara mrefu utakaofika mita 270.
Hivi sasa msikiti mrefu zaidi ni Msikiti wa Mfalme Hassan Wa Pili huko Casablanca Morocco ambao una mnara wenye urefu wa mita 210.
Msikiti huo ambao umepewa jina la Msikiti wa Jamia wa Algiers utajengwa katika ardhi yenye ukubwa wa hekari 20 na ujenzi wake unatekelezwa na shirika la China State Construction Engineering Corporation. Mradi huo unatazamiwa kumalizika mwaka 2015.
Waziri wa Masuala ya Kidini Algeria Bouabdallah Ghlamallah na Balozi wa China nchini humo Liu Yuhe walihudhuria sherehe za kuweka msingi msikiti huo Jumapili iliyopita.
Ukumbu wa sala katika msikiti huo utakuwa na nafasi ya watu 120,00 pamoja na maktaba yenye viti 2,000 mbali na jumba la makumbusho pamoja na kituo cha utafiti.
1015279
captcha