Shirika la habari la Syria SANA limetangaza kuwa, kundi la magaidi lilivamia nyumba za eneo hilo na kuzichoma moto kwa makusudi usiku wa Ijumaa na kisha kuvisingizia vikosi vya serikali kuwa ndivyo vilivyohusika na unyama huo. Katika upande mwingine Jenarali Robert Mood Mkuu wa Ujumbe wa Wasimamizi wa amani wa Umoja wa Mataifa nchini humo amesikitishwa na mauaji hayo na kuzitaka pande husika kukomesha mauaji ili kuutatua mgogoro wa kisiasa wa nchi hiyo. Wakati huo huo Bi. Catherine Ashton; Mkuu wa Siasa za Kigeni wa Umoja wa Ulaya amelaani vikali mauaji ya Hawlah, huku Uingereza nayo ikiitisha kikao cha dharura kwa lengo la kujadili suala hilo.
Nchi za Magharibi hasa Marekani na baadhi ya nchi za kieneo kama vile Qatar, Saudi Arabia na Syria zimetangaza wazi wazi kuunga mkono makundi ya kigaidi Syria ambayo yanataka kuiangusha serikali ya Rais Bashar Al Assad. Rais wa Syria anasakamwa kutokana na misimamo yake imara ya kuunga mkono harakati za ukombozi wa Palestina.
1019021