IQNA

Shakhsia ya Imam Hadi (as) yabainishwa huko India

17:14 - May 29, 2012
Habari ID: 2337183
Fadhila na sifa za kipekee za Imam Hadi (as) zimebainishwa katika kongamano lililofanyika siku ya Jumapili tarehe 27 Mei huko Lucknow katika jimbo la Uttar Pradesh nchini India.
Kongamano hilo limeandaliwa na Jumuiya ya Kitaifa ya Masuni wa India. Akibainisha sifa za Imam huyo mtukufu, Maulawi, Shahab ad-Deen mkuu wa jumuiya hiyo amesema kwamba sifa za kimaadili na kielimu za Imam huyo maasumu ni mfano bora wa kuigwa na Waislamu wote duniani. Ametaja baadhi ya hadithi kutoka kwa Imam Hadi kuhusiana na udharura wa kushukuru neema za Mwenyezi Mungu na kuongeza kuwa kushukuru neema ni muhimu zaidi kuliko neema yenyewe kwa sababu neema ni bidhaa inayomalizikia humu duniani lakini shukrani ni neema ya kudumu milele itakayoendelea kuwepo hadi Siku ya Kiyama. Shah Faisal, Shah Kalimullah, Haj Swalah Deen na Minhaj Ali ni wasomi na wanafikra wengine wa Kiislamu waliozungumza katika kongamano hilo na kubainisha fadhila za kimaadili na maisha ya Imam Hadi au kwa lakabu nyingine Imam Naqi (as) na jinsi alivyokuwa akiwanufaisha watu na mafundisho ya Kiislamu. Matatizo na mateso aliyokabiliana nayo Imam Hadi kutoka kwa watawala wa wakati huo ni mambo mengine yaliyotajwa kwenye kongamano hilo. 1018603
captcha