IQNA

Mashindano ya Qur'ani kwa wanafunzi wa kidini kufanyika Iraq

17:14 - May 29, 2012
Habari ID: 2337184
Mashindano ya kwanza ya kitaifa maalumu kwa wanafunzi wa kidini nchini Iraq yamepangwa kufanyika nchini humo Juni Mosi.
Mashindano hayo yameandaliwa na Dar al-Qur'an inayofungamana na Idara ya Haram ya Imam Hussein (as) katika mji mtakatifu wa Karbala. Mashindano hayo ambayo yamepangwa kufanyika kwa mnasaba wa maadhimisho ya Imam Jawad (as) hapo tarehe 10 Rajab yatafanyika katika makundi mawili ya hifdhi na kiraa ya Qur'ani. Kundi la hifdhi nalo litakawanywa katika makundi kadhaa ya hidhi ya Qur'ani nzima, hifdhi ya juzuu moja au zaidi na hifdhi ya baadhi ya sura za Qur'ani Tukufu za Yasin, al-Waqia na ar-Rahman. Sehemu ya mwisho ya mashindano hayo itakuwa ni ya kutangazwa washindi na kutunukiwa zawadi. Kila kundi litakuwa na washindi watatu na washindi wa kwanza katika makundi mawili ya hifdhi ya Qur'ani nzima na Kiraa watazawadiwa zawadi ya kufanya ziara ya umra mjini Makka, Saudi Arabia. Yule atakayeshinda katika kundi la hifdhi ya baadhi ya sura za Qur'ani, ataandaliwa fursa ya kuzuru Haram ya Imam Ridha mjini Mash'had Iran. Washindi wa pili na wa tatu wa kundi la hifdhi ya Qur'ani nzima na kiraa licha ya kupewa fursa ya kuzuru Haram hiyo pia watatunukiwa dinari laki moja za Iraq. Loho za kuwashukuru washindi pia zitatolewa.1018954
captcha