IQNA

Takwa la hijabu la wanawake wa Kiislamu wa Malawi

16:45 - May 30, 2012
Habari ID: 2337982
Jumuiya ya Wanawake wa Kiislamu wa Malawi MWO imemtaka Rais Joyce Banda wa nchi hiyo awaruhusu wanawake wa Kiislamu wa nchi hiyo kuvaa vazi la stara la hijabu katika ofisi za serikali nchini humo.
Kwa mujibu wa tovuti ya Islam Today, Fatuma Nadila, mkuu wa jumuiya iliyotajwa ya wanawake wa Kiislamu amekutana na kuzungumza hivi karibuni na Rais Joyce Banda wa Malawi na kumtaka afanye juhudi za kuruhusiwa wanawake wa Kiislamu wafanye kazi katika ofisi za serikali wakiwa wamevalia hijabu. Katika mazungumzo hayo, Banda amemuhakikishia Nadila kwamba anawaunga mkono kikamilifu wanawake wa Kiislamu na nafasi yao serikalini. Hivi karibuni wanawake wauguzi wa Kiislamu wameruhusiwa kutekeleza shughuli zao wakiwa wamevalia hijabu na vilevile wanawake hao wameruhusiwa kupiga picha za hati au pasi za kusafiria huku wakiwa wamevalia vazi hilo la heshima na la lazima kwa mwananke wa Kiislamu. Uislamu ni dini ya pili kwa ukubwa nchini Malawi ambapo takwimu rasmi za nchi hiyo zinaonyesha kwamba Waislamu wanaunda asilimia 12 ya jamii ya watu milioni 12 wa nchi hiyo ya Kiafrika. Hata hivyo Baraza la Waislamu wa nchi hiyo linalitilia shaka ukweli wa idadi hiyo na kusema kuwa idadi halisi ya Waislamu nchini humo ni asilimia 36 ya jamii yote iliyotajwa. 1020269
captcha