IQNA

Rais Ahmadinejad: Wanaadamu wanahitaji fikra za Imam Khomeini MA

9:55 - June 03, 2012
Habari ID: 2339627
Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema leo wanaadamu, zaidi ya wakati wowote ule, wanahitaji fikra, njia na malengo matakatifu ya Imam Khomeini MA.
Akizungumza Jumamosi usiku katika mkesha wa kumbukumbu ya mwaka wa 23 kuaga dunia Imam Khomeini MA muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Ahmadinejad ameongeza kuwa: ' Imam Khomeini MA aliamini kuwa malengo matukufu yanaweza kufikiwa kupitia utawala wa dunia wa Imam Mahdi ATF. Amesema katika maisha yake, Imam Khomeini alijitahidi kufikia lengo hilo tukufu. Katika hotuba hiyo aliyoitoa katika Haram Takatifu ya Imam Khomeini MA kusini mwa Tehran, Rais Ahmadinejad amesema karne hii , kwa uwezo wake Mwenyezi Mungu, itakuwa karne ya ushindi wa wanyonge dhidi ya mustakbirina. Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameendelea kusema kuwa, hayati Imam aliamini utawala wa madola ya istikbari ndio dhulma haribifu zaidi kwa wanaadamu na hivyo alisimama kidete dhidi ya mustakbirina. Ahmadinejad ameashiria pia mtazamo wa Imam Khomeini MA kuhusu utawala wa Kizayuni na kusema Imam alisimama kidete kuupinga utawala wa Kizayuni wa Israel ambao unadhulumu na kuyavunjia heshima mataifa na kumdhalilisha mwanaadamu.
1022570
captcha