IQNA

Mashia na Masuni wa Iraq walaani hujuma za kigaidi

13:10 - June 05, 2012
Habari ID: 2340337
Viongozi wa Mashia na Masuni nchini Iraq wametoa taarifa wakilaani vikali hujuma za kigaidi nje ya ofisi ya taasisi moja ya Kishia katika mji mkuu wa nchi hiyo Baghdad.
Katika mlipuko wa bomu huko Baghdad siku ya Jumatatu karibu watu 32 waliuawa .
Mlipuko huo ulitokea karibu na ofisi za iadara ya Waqfu wa Mashia katika eneo la Babul Muadham lililoko mjini Baghdad ambapo wengine wapatao 100 walijeruhiwa. Katika tukio hilo la kigaidi nyumba kadhaa za idara hiyo pia zimeharibiwa huku wafanyakazi wengi wa idara hiyo wakiwemo polisi wa usalama wakiuawa. Kufuatia tukio hilo vikosi vya usalama vya mjini Baghdad vimezingira eneo la tukio hilo na kuanzisha uchunguzi ili kuwatia nguvuni waliohusika na tukio hilo la kigaidi.

Viongozi wa Kishia na Kisunni Iraq katika taarifa yao wametoa wito kwa Waislamu wa madhehebu yote Iraq kudumisha utulivu na kuwatahadharisha wasitumbukie katika mtego wa maadui.
Spika wa Bunge la Iraq Osama Al Najifi ambaye ni Msunni amewataka Wairaqi waungane kukabiliana na maadui wa taifa hilo.
1023012
captcha