Kuna shule 98 kama hizo mjini humo lakini ni nne tu kati ya hizo ndizo zinawaruhusu wanafunzi wa kike kuhudhuria masomo yao wakiwa wamevalia vazi hilo la heshima. Inasemekana kuwa shule mbili kati ya hizo pia kuanzia mwaka huu wa masomo zimekuwa zikiwazuia mabinti wa Kiislamu kuhudhuria masomo yao wakiwa wamevalia hijabu na hivyo kufanya idadi ya shule zinazowazuia wanafunzi kuhudhuria masomo wakiwa wamevalia vazi hilo la stara kwa mwanamke wa Kiislamu kufikia 96. Maeneo tofauti ya Ubelgiji hutekeleza sheria tofauti kuhusiana na mavazi yanayopasa kuvaliwa na wanafunzi. Kwa mfano tokea mwaka 2009 shule 700 za jimbo la Flanders zimepiga marufuku hijabu kwa wanafunzi wa shule hizo. 1023233