IQNA

Kufungamana na Uislamu, njia pekee ya saada duniani na akhera

12:46 - June 06, 2012
Habari ID: 2341083
Kwa mtazamo wa Imam Khomeini MA, njia pekee ya saada na heshima ya Waislamu duniani na kesho akhera ni kufungamana na mafundisho ya Uislamu.
Haya ni kwa mujibu wa Mshauri wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu katika masuala ya kimataifa Dkt. Ali Akbar Velayati alipohutubu katika 'Kongamano la Kimataifa la Imam Khomeini MA na Mwamko wa Kiislamu.'
Dkt. Velayati aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya nje wa Iran ameongeza kuwa Imam Khomeini MA aliutazama umoja wa Waislamu kama dharura kwa ajili ya kuangamiza ubeberu na kukabiliana na nchi za Magharibi.
Ameashiria matukio ya hivi sasa ya mwamko wa Kiislamu na kuyataja kuwa 'zama mpya za Uislamu na kurejea katika thamani za Kiislamu jambo ambalo litapelekea kutatuliwa matatizo ya ulimwengu wa Kiislamu'.
Dkt. Velayati ameongeza kuwa hii si mara ya kwanza kushuhudiwa mwamko wa Kiislamu kwani kila wakati uwezo wa Waislamu unapodidimia huibuka viongozi ambao huinua bendera ya heshima ya Uislamu.
Akifafanua kuhusu nukta zilizopelekea kujitokeza mwamko wa Kiislamu hivi sasa, amesema Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran na mafanikio yake katika miaka 33 iliyopita yamepelekea kuibuka mwamko wa Kiislamu pamoja na kuwepo njama za maadui.
Dkt. Velayati amesisitiza kuwa njia yoyote isiyokuwa ya Uislamu itafeli kuleta mabadiliko katika jamii. Ameongeza kuwa: 'Hautapata nchi yoyote ya Waislamu kutoka Afrika Magharibi hadi Kusini Mashariki mwa Asia ambayo imefikia malengo yake kwa kufuata mfumo wa kimagharibi.'
Kongamano la 'Imam Khomeini MA na Mwamko wa Kiislamu limefanyika Tehran ambapo limeandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran.
1023550
captcha