Katibu Mkuu wa OIC ametoa wito kwa watu wote wa Iraq kutumia hekima na kujitahidi kuleta umoja nchini Iraq katika kipindi hiki nyeti ambapo Iraq na nchi za eneo zinapitia kipindi kigumu.
Aidha ametaka Waislamu wote Iraq kuzingatia Mkataba wa mwaka 2006 wa Makkah ulioungwa mkono na OIC kwa lengo la kuzuia hitilafu za kimadhehebu na misimamo mikali. Ihsanoglu amesema OIC iko tayari kushirikiana na serikali ya Iraq na kuandaa kikao mjini Baghdad kwa lengo la kutafuta njia za kutekeleza Mkataba wa Makkah.
Katibu Mkuu wa OIC pia ametuma salamu zake za rambi rambi kwa familia za wahanga wa tukio hilo la kigaidi na kuwaombea shifaa waliojeruhiwa.
Karibu watu 33 waliuawa na wengine 100 kujeruhiwa katika milipuko hiyo ya Bagadad.
1024995