Kituo hicho kitaanzishwa na Jumuiya Injili ya Marekani. Kwa mujibu wa tovuti ya Chronical kituo hicho cha Qur'ani kitakuwa kituo huru kitakachojishughulisha na masuala ya utafiti wa Qur'ani na kutoa mafunzo ya Qur'ani katika nyanja tofauti za historia, dini na utamaduni. Kituo hicho pia kitakuwa kikijishughulisha na uchapishaji wa vitabu na majarida yanayohusiana na masuala ya Qur'ani na kutoa huduma za kitaalamu kwa watafiti wa Qur'ani. Akibainisha suala hilo John Cotsco, Mkurugeni Mwandamizi wa Jumui ya Injili ya Marekani amesema leo kuna haja kubwa ya kuifahamu Qur'ani na kwamba jamii ya leo haiwezi kujiita kuwa imestaarabika bila ya kuwa na habari za kutosha kuhusu kitabu hicho kitakatifu. Ripoti zinasema kuwa kuna ongezeko kubwa la watu wanaotaka kuujua Uislamu na kwamba lengo hilo haliwezi kufikiwa bila kuifahamu Qur'ani. Kwa msingi huo Qur'ani imekuwa kati ya vitabu vinavyonunuliwa kwa wingi katika nchi za Magharibi na hasa nchini Marekani. 1025819