Huku duru ya pili ya uchaguzi wa urais wa Misri ikikaribia, maelfu ya wananchi na wanaharakati wa kisiasa waliandamana siku ya Ijumaa katika medani ya Tahriri mjini Cairo kupinga kugombea Ahmad Shafiq kwenye duru hiyo ya uchaguzi, wakisema kuwa hawataki kuongozwa na afisa huyo wa zamani wa jeshi.
Waandamanaji hao ambao pia wamemuunga mkono mgombea wa Ikhwanul Muslim katika uchaguzi huo Muhamed Morsi pia wametahadharisha juu ya njama ya baraza la kijeshi la nchi hiyo ya kutaka kumsaidia Shafiq aingie madarakani.
Uchaguzi huo wa duru ya pili ya urais utakaofanyika Juni 16 na 17 nchini Misri ni hatua ya mwisho ya kukabidhi uongozi wa nchi hiyo kwa serikali ya kiraia, baada ya jeshi kushika madaraka kufuatia wananchi wa nchi hiyo kuupindua utawala wa dikteta Hosni Mubaraka.
Watawala wa kijeshi watakabidhi madaraka kwa rais mpya atakayechaguliwa na wananchi tarehe Mosi mwezi ujao wa Julai.
1025696