IQNA

Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Iran yaimarisha umoja wa Waislamu

13:40 - June 10, 2012
Habari ID: 2343323
Mwanazuoni wa ngazi za juu nchini Iran Ayatullah Sayyed Ahmad Khatami amesema mashindano ya kimataifa ya Qur'ani yana mchango mubwa katika kuimarisha umoja wa Waislamu duniani.
Kwa mujibu wa tovuti ya Shirika la Awqaf la Iran, Ayatullah Khatami ambaye pia ni mwanachama wa Baraza la Wanazuoni Wataalamu Wanaomchagua Kiongozi Muadhamu, ameongeza kuwa, kwa kuandaa mashindano ya kimataifa ya kuhifadi na kusoma Qur'ani, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaweza kueneza ujumbe wa kweli duniani.
Amesema kuna umuhimu wa kueneza fikra za Qur'ani duniani na amepongeza juhudi za Shirika la Awqaf Iran kwa kuchukua hatua muafaka katika suala hili.
Ayatullah Khatami ameashiria kutarujumiwa Qur'ani Tukufu kwa lugha mbali mbali na kusema hiyo ni kati ya hatua muhimu zilizochukuliwa na shirika hilo katika kusambaza mafundisho ya Qur'ani.
Mwanazuoni huyo amesema Qur'ani Tukufu ndio mhimili bora zaidi wa kuleta umoja na mshikamano miongoni mwa Waislamu duniani.
1025464
captcha