IQNA

Mashindano ya Qur'ani ni ishara ya Iran kufungamana na Hadithi ya Thaqalain

18:57 - June 11, 2012
Habari ID: 2344204
Hatua ya Iran kuandaa mashindano kadhaa ya kimataifa ya Qur'ani yakiwemo ya wanafunzi wa vyuo vikuu ni ishara ya kutekelelza Hadithi ya Thaqalain ambayo inawataka Waislamu wategemee Qur'ani Tukufu na Ahlul Bayt AS.
Haya ni kwa mujibu wa Mohammad Masoud Ismaili mwanaharakati maarufu wa Qur'ani nchini Iran. Katika mahojiano na IQNA, ameongeza kuwa mashindano kadha aya kimataifa yanayofanyika Iran kila mwaka ni katika ya hafla bora zaidi za Qur'ani katika Ulimwengu wa Kiislamu. Amesema pia hatua ya Iran kutuma maqari na mahufadh wa Qur'ani sehemu mbali mbali duniani ni ishara ya kuimarika kiwango cha ujuzi wa Qur'ani nchini.
'Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Wanachuo Waislamu ambayo yameandaliwa na Shirika la Iran la Harakati za Qur'ani za Wanafunzi- ISQAQ ni jambo ambalo linaashiria kiwango cha harakati za Qur'ani nchini,' amesema.
Ameendelea kusema kuwa wale wanaofanikiwa katika mashindano ya Qur'ani hawategemeii tu uwezo wao bali huweza kufuzu kutokana na utamaduni wa Qur'ani unaotawala kote Iran.
1025778
captcha