Kwa mujibu wa tovuti ya guysen, Said Hamam ambaye ni kiongozi wa Ikhwanul Muslimin ya Jordan ameongoza ujumbe wa zaidi ya wanaharakati 100 wa Kiislamu wa nchi hiyo katika safari yake hiyo katika Ukanda wa Gaza. Ujumbe huo umewapelekea misaada ya madawa wakazi wa ukanda huo ambao wanakabiliwa na matatizo mengi kutokana na mzingiro wa kidhulma unaotekelezwa dhidi yao na utawala haramu wa Israel. Ujumbe huo umetoa taarifa ukimuhutubu Ismail Hania Waziri Mkuu wa serikali ya Palestina kwa kusema kwamba wasikate tamaa na kudhani kwamba wako peke yao katika mapambano yao dhidi ya dhulma ya utawala haramu wa Israel na kutaka kuvunja mzingiro uliotajwa, bali ndugu zao wa Jordan wako pamoja nao katika mapambano yao hayo. 1027334