Kwa mujibu gazeti linalochapishwa nchini humo la Tribune, bomu lililokuwa limetegwa kwenye pikipiki iliyokuwa imeegeshwa karibu na barabara lililipuliwa mara tu baada ya basi hilo kufika mahala hapo. Nasibullah Bazai mmoja wa viongozi wa Quetta amesema bomu hilo lililipuliwa kutokea mbali na kwamba uchunguzi wa maafisa wa usalama bado unaendelea.
Wafanya ziara hao walikuwa wakielekea nchi jirani ya Iran kwa lengo la kufanya ziara. Hadi sasa hakuna kundi lolote la kigaidi ambalo limetangaza kuhusika na shambulio hilo.
Mashambulio ya kigaidi dhidi ya Waislamu wa madhehebu ya Shia yamekuwa yakiongezeka katika miaka ya hivi karibuni nchini Pakistan, moja ya sababu ikiwa ni kuongezeka kwa shughuli za kigaidi za Mawahabi na propaganda dhidi ya Waislamu wa Kishia nchini humo. 1028109