IQNA

Harakati ya Hizbullah inatetea umoja

12:43 - June 14, 2012
Habari ID: 2346317
Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah nchini Lebanon amesema harakati hiyo ya mapambano inasisitiza kuhusu kutetea mashalhi ya kitaifa na umoja wa ili kudumisha usalama nchini humo.
Akizungumza Jumanne Juni 12 wakati alipokutana na Haj Ahmad Ghandour Mkuu wa Jumuiya ya Kukurubisha Madhehebu ya Kiislamu Lebanon, Sheikh Naeem Qasseim amesema Hizbullah ina azma ya kukabiliana na hatari iliyopo katika eneo yaani sera za utawala haramu wa Israel za kukalia kwa mabavu ardhi za wengine.
Amesisitiza haja ya Walebanon wote kuungana katika kuimarisha harakati ya Hizbullah, kuimarisha maisha ya wananchi na kuzuia hitilafu za kikaumu na kimadhehebu. Sheikh Naeem Qassim amesisitiza kuhusu umuhimu wa umoja nchini Lebanon na ametoa wito kwa wanasiasa vigogo na viongozi wa makundi mbalimbali nchini humo kujiepusha na hotuba zinazovuruga umoja na mshikamano.
Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah amesema kuwa kudumisha umoja ni jambo la lazima ili kukabiliana na vitisho vya kigeni.
1028974
captcha