IQNA

Sira ya Mtume (saw) yachunguzwa katika kongamano la Uturuki

18:06 - June 16, 2012
Habari ID: 2347932
Sira na mwenendo wa Mtume Muhammad (saw) vimechunguzwa katika kongamano lililofanyika tarehe 13 Juni katika Chuo Kikuu cha Batban nchini Uturuki.
Ripota wa IQNA amesema kuwa kongamano hilo la kidini lilihudhuriwa na wanafunzi wa vyuo vikuu na kuhutubiwa na mwandishi na mhakiki wa sayansi za Kiislamu nchini Uturuki Muhammad Amin Yildirim.
Msomi huyo ambaye amefanya uhakiki kwa miaka mingi kuhusu sayansi na elimu za Kiislamu amesisitiza juu ya udharura wa kutegemewa sira na maagizo ya Mtume Muhammad (saw) katika masuala yote ya maisha.
Mwandishi huyo wa Kiislamu wa Uturuki ameashiria kipindi cha mwanzoni mwa Uislamu na maisha ya zama hizo na kufanya ulinganisho wa kipindi hicho na zama za sasa. 1031123

captcha