IQNA

Sherehe za kubaathiwa Mtume (saw) kufanyika kesho Kigali

16:41 - June 17, 2012
Habari ID: 2348823
Sherehe za kuadhimisha siku aliyopewa utume na kubaathiwa Nabii Muhammad (saw) zimepangwa kufanyika kesho Jumatatu tarehe 27 Rajab katika Msikiti wa Imam Ali (as) katika eneo la Remera mjini Kigali Rwanda.
Sherehe hizo zimetayarishwa na Waislamu wa madhehebu ya Shia na zitaanza alasiri hadi wakati wa Swala za magharibi na Ishaa.
Sherehe hizo zitahutubiwa na maulamaa wa Kislamu wa madhehebu ya Shia na kuhudhuriwa na Waislamu hususan Mashia kutoka kote nchini humo.
Sheikh Hassan Bagaruka ambaye ni imam wa Msikiti wa Imam Ali (as) amepangiwa kuzungumzia sifa na sira ya Mtume Muhammad (saw) katika sherehe hiyo. 1032162
captcha