Akizungumza na IQNA, Ahmed Mersad Ilyas amesema amekuwa akitizama mashindano ya miaka iliyopita kwa njia ya televisheni na kuongeza kuwa uzoefu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kuandaa mashindano unaimarika kila mwaka.
Amesema kuandaa mashindano ya Qur’ani pia husaidia kuarifisha Iran kwa Waislamu wa nchi zingine na hivyo kuvunja njama za kueneza chuki dhidi ya Iran katika nchi za Magharibi.
‘Inatazamiwa kuwa, wanaporejea makwao, washirikia wa mashindano ya Qur’ani watafikisha ujumbe kuhusu ukweli wa mambo katika Jamhuri ya Kiislamu na hivyo kubatilisha propaganda zilizopo kuhusu nchi hii.’
Ameongeza kuwa amewahi kutembelea Iran na kuzuru maeneo matakatifu ya haram ya Imam Reza AS.
Kuhusu harakati za Qur’ani Ujerumani, Mersad Ilyas ambaye anaishi Hamburg amesema vijana Waislamu wana hamu ya kujifunza Qur’ani lakini tatizo ni kuwa waalimu wa Qur’ani ni wachache.
Mashindano ya 29 ya Kimataifa ya Qur’ani yanaendelea katika Mnara wa Miladi mjini Tehran na yatamalizika Juni 22.
1034052