IQNA

Vitabu vya Kiislamu vyapigwa marufuku Ufaransa

13:32 - June 25, 2012
Habari ID: 2353601
Duka pekee la vitabu vya Kiislamu katika mji wa Annecy Ufaransa limefungwa kwa amri ya manispaa ya mji huo.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Issa Bulksibet ambaye ni mkurugenzi wa Duka la Vitabu katika mji wa Annecy amesema uamuzi huo umechukuliwa kufuatia uchochezi wa wauza vitabu kadhaa katika eneo hilo ambao wametaka marufuku ya uuzwaji vitabu vya Kiislamu mjini humo.
Amesema Manispaa ya Annecy imepiga marufu uuzaji vitabu vya Kiislamu kwa lengo la kuzuia kuenezwa mafunzo ya Kiislamu na kukabiliana na ongezeko la Wafaransa wanaosilimu.
Bulksibet amekosoa uamuzi huo ambao ameutaja kuwa ulio kinyume cha sheria na wenye chuki dhidi ya Uislamu. Amesema anaamini Meya wa mji huo amewapuuza raia Waislamu walio wachahce ambao wanahitaji vitabu vya Kiislamu.
Hivi karibuni Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limelaani vikali ubaguzi unaofanywa dhidi ya Waislamu barani Ulaya na jinsi chuki dhidi ya Uislamu zinavyotumiwa kwa ajili ya maslahi ya kisiasa.
Ripoti ya Amnesty International imejikita zaidi kuhusu hali ya Waislamu katika nchi za Ufaransa, Ubelgiji, Uholanzi, Uhispania na Uswisi na kuzitaka nchi za Ulaya kukabiliana na ubaguzi dhidi ya Waislamu hususan katika taasisi za elimu na maeneo ya kazi.
Ufaransa ndio nchi yenye idadi kubwa zaidi ya Waislamu barani Ulaya ambapo kuna karibu Waislamu milioni tano hadi sita na idadi hiyo inaongezeka kwa kasi. Hivi sasa Uislamu ndio dini ya pili kwa idadi nchini Ufaransa.
1035246
captcha