Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Kamati ya Turathi za Dunia yenye wanachama 21 ilitangaza uamuzi huo katika kikao chake cha 36 huko St. Petersburg, Russia.
Msikiti wa Jamia wa Isfahan ambao ulijengwa mwaka 771 Miladia ndio wa kale wa aina yake uliohifadhiwa Iran na muundo wake umeigwa katika ujenzi wa misikiti mingine kote katikati mwa Asia.
Msikiti wa Jamia wa Isfahan ambao pia unajulikana kwa jina la Masjid Atiq ndio jengo la kwanza la Kiislamu ambalo lilitumia muundo wa maeneo manne ya wazi.
Hadi sasa maeneo 14 ya Iran yamewekwa katika orodha ya dunia ya UNESCO. Kamati ya Turathi za Dunia pia inatazamiwa kuchunguza pendekezo la kuwekwa Quba ya Qabus au Gonbad-e-Qabus katika orodha ya turathi za dunia.
1041911