Huku ziku za Nusu-Shaaban na sherehe za maadhimisho ya kuzaliwa Imam Mahdi (af) zikiwa zinakaribia, hatua maalumu za usalama zinachukuliwa katika mji mtakatifu wa Karbala kwa madhumuni ya kulinda usalama wa waumini na wageni watakaofanya ziara katika mji huo.
Kwa mujibu wa tovuti ya Saut al-Iraq, Kamati ya Masuala ya Usalama ya Karbala imesema kuwa kikosi maalumu cha askari usalama kitatekeleza taratibu maalumu za kiusalama kwa madhumuni ya kulinda maisha ya watu na wafanyaziara katika mji huo ambao una haram za watukufu wawili wa Kiislamu, Imam Hussein na Abulfadhl al-Abbas (as) kwa lengo la kusherehekea uzawa wa Imam wa 12 wa Mashia, Imam Mahdi (as).
Kamati hiyo imesema kwamba kikao hicho kitajumuisha askari 33,000 kutoka jeshi, polisi na vikosi vingine maalumu vya kulinda usalama. Imeongeza kuwa kikosi hicho pia kitajumuisha jeshi la anga.
Wakati huohuo Wizara ya Ulinzi ya Iraq imetangaza kwamba askari usalama wameafanikiwa kutia mbaroni makundi mawili ya kigaidi yanayofungamana na mtandao wa al-Qaida ambayo yalihusika na mauaji na ulipuaji mabomu kusini mwa mji mkuu Baghdad. 1041337