Kongamano hilo ambalo litaanza July 14 litawaleta pamoja wanaharakati wanawake Waislamu kutoka kote duniani hasa nchi za Kiislamu.
Mkutano huo utajadili nafasi muhimu ya wanawake katika mchakato wa Mwamko wa Kiislamu ulioshuhudiwa Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini.
Waandishi habari 50 wa nchi za kigeni watafika Tehran kwa lengo la kuakisi habari za kongamano hilo la siku mbili, amesema Mohammad Javad Aghajari mkurugenzi wa vyombo vya habari vya kigeni katika Wizara ya Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu. Aghajari ameongeza kuwa wawakilishi 150 wa vyombo vya habari vya kigeni mjini Tehran pia wataakishi habari za mkutano huo ambao utamalizika Julai 15.
Mapema mwezi wa Januari mwaka huu mji wa Tehran ulikuwa mwenyeji wa Kongamano la Kimataifa la Vijana na Mwamko wa Kiislamu ambapo wasomi 1500 kutoka nchi 73 walishiriki. Aidha wanaharakati 700 wa Kiislamu kutoka nchi 80 walishiriki katika Kongamano la Kwanza la Mwamko wa Kiislamu lililofanyika Septemba mwaka 2011.
1043075