Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Michel D'Hooghe Mkuu wa Kamati ya Afya amesema, ‘matatizo niliyokuwa nayo kuhusu vazi la Hijabu yalikuwa ya usalama wa kiafya na sasa sina mushkili na hilo tena.’
Amesema imebainika kuwa hakuna hatari ya kunyongwa kwa anayevaa hijabu na kucheza mpira kwa hivyo vazi hilo halina hatari.
Hijabu zilipigwa marufuku katika mashindano ya FIFA mwaka 2007 kwa madai kuwa zinahatarisha usalama wa kiafya wa wachezai. Mwezi Machi mwaka 2012 Bodi ya Kimataifa ya Soka IFAB iliwaruhusu wanawake waislamu kuvaa vazi la hijabu.
Aprili mwaka huu FIFA ilitangaza kuwa itapiga marufuku uvaaji hijabu katika michezo ya Olimpiki ya mwaka 2012 mjini London.
Mwaka jana Timu ya Soka ya Wanawake ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilizuiwa kushiriki katika raundi ya pili ya michezo ya kufuzu katika michezo ya Olimpiki dhidi ya Jordan baada ya kukataa kuvua hijabu zao.
Iran ambayo ilikuwa inaongoza kundi hilo ilikoseshwa fura ya kushiriki katika michezo ya Olimpiki London kutokana na marufuku hiyo.
1042302