IQNA

Kipindi cha kuogopwa Israel nchini Misri kimeisha

17:29 - July 03, 2012
Habari ID: 2360064
Muhammad al-Baltaji, Katibu wa Chama cha Uhuru na Uadilifu, ambacho ni tawi la kisiasa la Harakati ya Ikhwanul Muslimin nchini Misri amesema utawala haramu wa Israel unapasa kutambua kwamba kipindi cha serikali ya Misri kuuogopa kimefikia ukingoni.
Kwa mujibu wa tovuti ya Almanar, katibu huyo huku akisisitiza kwamba serikali mpya ya Misri haina nia ya kuzusha mvutano na kundi wala serikali yoyote ameongeza kuwa hata hivyo utawala haramu wa Israel unapasa kutambua kwamba kipindi ambacho utawala huo ulikuwa ukitoa mashinikizo dhidi ya utawala wa Mubarak na kuzusha hofu miongoni mwa wananchi wa Misri kimefikia ukingoni.
Muhammad al-Baltaji amesema suala la kuingia na kutoka Wazayuni katika jangwa la Sinai la Misri bila kupata vibali rasmi kutoka kwa serikali ya Cairo litachunguzwa upya kwa sababu ni jambo linalohatarisha usalama wa Misri. 1043999
captcha