Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, wakuu wa mji wa Madina wamesema watu ambao milki zao zitachukuliwa kwa ajili ya upanuzi wa msikiti huo watakuwa wameshalipwa fidia kabla ya kuanza ukarabapi.
Imekadiriwa kuwa fidia hiyo itagharimu bilioni 25 Riali za Saudia kwa wanaomiliki ardhi au majengo katika eneo lenye ukubwa wa ekari 12.5
Kati ya majengo yatakayobomolewa katika upanuzi huo ni Hospitali ya Wanawake, hoteli kadhaa, jengo la Ashqi, jengo nambari 2 la awqaf na jengo la al Muhamadia Waqf katika eneo la mashariki.
Mradi huo wa upanuzi utatekelezwa katika awamu tatu. Awamu ya kwanza itakuwa na eneo lenye uwezo wa kubeba watu 800,000 na awamu ya tatu itaongeza idadi ya waumini hadi milioni moja laki sita.
1044224