Kwa mujibu wa Press TV, abiria 18 waliokuwemo kwenye basi hilo waliuawa katika shambulio hilo lililotekelezwa jana asubuhi katika eneo la Kach katika mji wa Turbat katika mkoa wa Baluchestan.
Shambulio hilo lililotekelezwa na magaidi waliokuwa wanaendesha pikipiki pia lilijeruhi watu wengi.
Parviz Ashraf, Waziri Mkuu wa Pakistan ametoa taarifa akilaani shambulizi hilo na kusisitiza kwamba halitadhoofisha irada na uamuzi wa serikali wa kupambana na magenge ya kigaidi yanayotoa ovyo roho za watu wasio na hatia.
Mashia wa Pakistan pia wamelaani ugaidi huo na kuitaka serikali ibuni tume ya uchunguzi haraka iwezekanavyo ili kushughulikia suala hilo.
Katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita magenge ya kigaidi na hasa ya Kiwahabi yamekuwa yakiwalenga Mashia ambapo kufikia sasa yameua maelfu miongoni mwao. Mashirika mengi ya kutetea haki za binadamu ya Pakistan pia yamelaani mauaji hayo dhidi ya raia wasio na hatia. 1046552