IQNA

Mashindano ya Qur'ani Dubai kufanyika Mwezi wa Ramadhani

11:46 - July 08, 2012
Habari ID: 2363173
Mashindano ya 16 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu yenye anwani ya 'Zawadi ya Dubai' yataanza katika siku ya kwanza ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani mwaka huu wa 1433 Hijria Qamaria.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mashindano hayo yatafanyika kwa himaya ya Kamati ya Kuandaa Zawadi ya Kimataifa ya Qur'ani ya Dubai katika Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati).
Kamati andalizi imetoa taarifa na kusema mipango ya kuandaa mashindano hayo ya Qur'ani inakaribia kukamilika
Taarifa hiyo imesema pembizoni mwa mashindano hayo kutakuwa na semina na vikao kwa lugha za Kiingereza, Kiarabu na Kiurdu kuhusu Qur'ani Tukufu.
Mashindano hayo yatawakutanisha pamoja washiriki kutoka nchi za Kiarabu na Kiislamu na nchi zisizo za Kiislamu zenye Waislamu wachache.
Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu yenye anwani ya 'Zawadi ya Dubai' yalianza mwaka 1418 Hijria Qamaria sawa na mwaka 1997 Miladia na yametajwa kuwa mashindano marefu zaidi ya Qur'ani duniani.
1047312


captcha