IQNA

Waislamu wa Indonesia walalamikia marufuku ya Swala ya Ijumaa

13:06 - July 09, 2012
Habari ID: 2364201
Waislamu wa Surabaya mji wa pili kwa ukubwa nchini Indonesia wamefanya maandamano mbele ya jingo la shirika la Hasil Fastindo mjini humo lililowafukuza kazi wafanyakazi wake wa Kiislamu kwa kuhudhuria Swala ya Ijumaa.
Maandamano hayo yamefanyika baada ya shirika hilo kuchukua hatua ya kuwafukuza kazi wafanyakazi wake 24 kwa kuhudhuria Swala ya Ijumaa katika msikiti wa ijumaa mjini humo.
Waandamanaji wamekosoa vikali hatua ya shirika hilo na kulitaka liheshimu uhuru wa kuabudu wa wafanyakazi wake. Wamesema kutokana na kuwa Indonesia inatambua haki za ibada za wananchi wa nchi hiyo shirika hilo halipasi kuzikanyaga haki hizo kwa kuwazuia wafanyakazi wake kutekeleza ibada hizo.
Jambo la kushangaza hapa ni kuwa licha ya kuwa Indonesia ni nchi ya Kiislamu na iliyo na idadi kubwa zaidi ya Waislamu duniani lakini inafuata misingi na utamaduni wa nchi za Kikristo na kufanya siku za Jumamosi na Jumapili kuwa siku za mapumziko badala ya siku ya Ijumaa. Jambo hilo limepelekea wafanyakazi wengi wa Kiislamu wanaofanya kazi katika mashirika yasiyo ya Kiislamu kukabiliwa na matatizo. 1048313
captcha