Waandamanaji hao pia wameelezea kufungamana kwao na Sheikh Nemr ambaye gari lake lilifyatuliwa risasi na wanajeshi ambao walimtia mbaroni Jumapili katika eneo la Qatif, mashariki mwa Saudi Arabia.
Wakati huo huo watu watatu wamepigwa risasi na kuuawa na vikosi vya Saudi Arabia katika maandamano yaliyofanyika hapo jana nchini humo. Habari zinasema kuwa, maandamano hayo yaliitishwa kupinga hatua ya serikali ya nchi hiyo ya kumkamata Sheikh Al Namr.
Kwa siku kadhaa sasa wananchi wa Saudia wamekuwa wakifanya maandamano katika maeneo tofauti ya nchi hiyo wakiitaka serikali ya Riyadh kuwaachilia huru wafungwa wa kisiasa ambao wamekuwa wakishikiliwa katika korokoro za jeshi la nchi hiyo kwa muda mrefu bila ya kushtakiwa.
1048456