IQNA

Harakati za Qur’ani kuimarika zaidi Iran

14:15 - July 11, 2012
Habari ID: 2366048
Mkuu wa Maonyesho ya 20 ya Kimataifa ya Qur’ani ya Iran amesema kuwa katika siku za usoni kutashuhudiwa ongezeko kubwa la harakati za Qur’ani.
Akizungumza Jumanne mjini Tehran katika kikao cha kuratibu maonyesho ya Qur’ani, Sheikh Hamid Mohammadi ameashiria hatua ya serikali kutenga kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya shughuli za Qur’ani nchini na kuongeza kuwa inatazamiwa kuwa katika mustakabali wa karibu harakati za Qur’ani zitakuwa mara kadhaa zaidi ya kipindi chote cha miongo mitatu iliyopita.
Sheikh Mohammadi ambaye pia ni Naibu Waziri wa Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu anayesimamia masuala ya Qur’ani amesema maonyesho yajao ya kimataifa ya Qur’ani ni ya wananchi na kwamba wizara yake ni mratibu tu wa maonyesho.
Ameendelea kusema kuwa maonyesho ya kimataifa ya Qur’ani Tehran ndio makubwa zaidi ya aina yake duniani na ameongeza kuwa Iran iko tayari kuandaa maonyesho kama hayo katika nchi za Kiislamu.
Maonyesho ya 20 ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu Iran yataanza Julai 15 katika ukumbi wa Sala wa Imam Khomeini SA.
1049859
captcha