IQNA

Mkutano wa Wanawake na Mwamko wa Kiislamu kumalizika leo Tehran

17:21 - July 11, 2012
Habari ID: 2366430
Mkutano wa kwanza wa kimataifa wa Wanawake na Mwako wa Kiislamu unaoendelea mjini Tehran unakamilisha shughuli zake leo kwa kusomwa taarifa ya mwisho ya washiriki katika mkutano huo.
Mkutano huo ambao ulinza jana kwa hotuba ya Rais Mahmoud Ahmadinejad unahudhuriwa na wasomi na wanaharakati wa kike kutoka nchi mbalimbali na utakamilika kwa kusomwa taarifa ya mwisho na kuarifishwa makala bora zaidi.
Makala zilizowasilishwa katika mkutano huo wa kwanza wa kimataifa wa Wanawake na Mwamko wa Kiislamu zilijadiliwa jana katika kamati sita za wataalamu zilizojadili 'fikra za Kiislamu na mwamko wa Kiislamu", uwezo wa wanawake na kazi za kimapinduzi", "wanawake na mwamko wa Kiislamu, fursa, vitisho na njia za utatuzi", "mafanikio na mahitaji", familia na uwezo wa kutengeneza wanawapinduzi" na "mustakbali na mabadiliko yajayo".
Mkutano wa kwanza wa kimataifa wa Wanawake na Mwamko wa Kiislamu unahudhuriwa na zaidi ya wanawake 1200 wanaharakati katika nyanja mbalimbali za kisiasa, kijamii na vyombo vya habari kutoka nchi 85 duniani. 1050118

captcha