Kwa mujibu wa tovuti ya Islam Times, viongozi wa Palestina wanasema uamuzi wa ICJ ulikuwa muhimu sana kwani ulimaanisha kuwa ujenzi wa vitongozi vya Wazayuni pamoja na ukuta huo wa kibaguzi ni kinyume cha sheria.
Hata hivyo Wapalestina wanasikitika kuwa jamii ya kimataifa hasa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Ulaya hazijachukua hatua za kutosha kutekeleza uamuzi wa ICJ.
Malalamiko ya raia wa Palestina katika kupinga siasa za kibaguzi za utawala wa Kizayuni wa Israel huko katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na utawala huo yameongezeka katika kipindi hiki cha kukumbuka siku ulipotolewa uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu ICJ ya mjini Hague Uholanzi wa kulaani hatua ya utawala wa Kizayuni ya kujenga ukuta wa kibaguzi katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu.
Kwa kujenga ukuta huo wa kibaguzi, utawala wa Kizayuni wa Israel umedhihirisha waziwazi utambulisho wake halisi uliobuniwa kwa misingi ya kibaguzi na ukandamizaji. Vitendo vya kupenda kujitanua vya utawala wa Kizayuni kama vile ujenzi wa ukuta wa kibaguzi na vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi katika ardhi za Wapalestina vinakinzana waziwazi na maazimio ya Umoja wa Mataifa na makubaliano ya kimataifa.
1053123