Waandamanaji hao walikusanyika nje ya Ikulu ya Rais siku ya Jumamosi wakati Clinton akipokuwa akifanya mazungumzo na Rais Mohammad Morsi.
Wakati msafara wa Clinton ulipoondoka katika Ikulu ya Rais, waandamanaji walijipanga barabarani na kutoa nara dhidi ya Marekani. Wamisri wanapinga njama za Marekani za kuidhibiti nchini hiyo wakisema kuwa Washington inapanga njama ya kuigawa Misri vipande vipande.
Aidha Wamisri wamesema wanapinga mkakati wa Marekani wa kuikurubisha Misri na utawala haramu wa Israel.
Maandamano makubwa pia yamefanyika nje ya Ubalozi wa Marekani mjini Cairo wakati Clinton alipokuwa anawahutubia waandishi habari.
Vifaru vya jeshi la Misri vimeonekana nje ya ubalozi huo wa Marekani sehemu ambayo imekuwa medani ya maandamano dhidi ya Marekani tokea uanze mwamako wa Kiislamu wa Wamisri uliopelekea kutimuliwa madarakani dikteta Hosni Mubarak mwaka 2011.
1052923