IQNA

Njama ya kutaka kumuua Ayatullah Sistani yavunjwa

12:49 - July 17, 2012
Habari ID: 2370793
Chombo kimoja cha kuaminika kiusalama katika mji mtakatifu wa Najaf nchini Iraq kimesema kwamba gaidi mmoja aliyekuwa na nia ya kushambulia nyumba ya Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Sistani kwa lengo la kutaka kumuua kigaidi mwanazuoni huyo mashuhuri wa Kishia amekamatwa.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Infirad la nchini Kuwait, gaidi huyo aliyekuwa amejifunga mkanda wa mada za milipuko alikamatwa akiwa nje ya nyumba ya mwanazuoni huyo tayari kutekeleza jinai dhidi yake.
Akizungumzia suala hilo Hamid al Khafaf, msemaji wa ofisi ya Ayatullah Sistani mjini Beirut Lebanon amesema kuwa gaidi huyo mkazi wa Najaf aliye na umri wa miaka 39 alikamatwa siku ya Jumapili. Al-Khafaf amesema kuwa gaidi huyo alikuwa ametaka kuonana mara kadhaa na Ayatullah Sistani kwa hoja ya kutaka kumuomba fedha za kumtibu binti yake lakini ombi lake lilikataliwa kwa sababu mwanazuoni huyo alikuwa hajisikii vizuri kiafya.
Habari zaidi kutoka Najaf zinasema kwamba askari usalama wa mji huo mtakatifu walizuia kusambazwa kwa habari hiyo kupitia vyombo vya habari kwa lengo la kulinda usalama wa mkoa wa Najaf katika siku hizi muhimu za kukaribia mwezi mtukufu wa Ramadhani. 1054706
captcha