IQNA

Israel yaonywa kuhusu kuuvamia Msikiti wa Al Aqsa

15:18 - July 18, 2012
Habari ID: 2371699
Tume ya Kiislamu na Kikristo huko Palestina imeonya kuhusu natija ya matamshi yaliyotolewa hivi karibuni na Yehuda Feinstein mshauri wa kisheria wa utawala haramu wa Israel aliyedai kuwa eti Msikiti wa Al Aqsa ni sehemu isiyotenganika ya Wazayuni.
Tume hiyo imeonya kuwa matamshi kama haya yanaupa utawala wa Kizayuni wa Israel kiburi cha kuendelea kuuharibi Msikiti wa Al Aqsa na kuupa sura bandia ya Kiyahudi.
Tume hiyo imemtaka Papa Bendict XVI, nchi zote za Kiarabu na Kiislamu pamoja na taasisi kama vile Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu kuchukua hatua za haraka kuunusuri Msikiti wa Al Aqsa kutokana na hujuma ya utawala ghasibu wa Israel.
Wakati huo huo kufuatia matamshi hayo ya Yehuda Feinstein Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imesisitiza kuwa, umma wa Kiislamu kamwe hautakubali kuvamiwa na kukaliwa kwa mabavu msikiti wa al Aqsa.
Profesa Ekmeleddin Ihsanoglu, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya OIC yenye makao yake katika mji wa Jeddah wa Saudi Arabia, amelaani madai ya viongozi wa utawala wa Kizayuni kwamba msikiti wa al Aqsa ni sehemu isiyotenganishika na ardhi inazozikalia kwa mabavu na kusisitiza kuwa umma wa Kiislamu kamwe hautakubali kuvamiwa na kukaliwa kwa mabavu msikiti huo.
Katibu Mkuu wa OIC amesema msikiti wa al Aqsa ni kibla cha kwanza cha Waislamu na ni moja ya maeneo matukufu kwa umma wa Kiislamu na amewataka mabalozi wa nchi za Kiislamu katika shirika la kimataifa la UNESCO kuchukua hatua haraka iwezekanavyo kusitisha uvamizi wa Israel katka maeneo ya kidini na ya kihistoria ya mji mtukufu wa Quds..

1056315
captcha