Ali Akbar Salehi alisema hayo Jumanne mjini Tehran katika wa mkutano wa awali wa kitaalamu na kimataifa wa NAM ulifanyika na kuongeza kuwa NAM pia inapaswa kutumia uwezo wake katika kutatua mizozo ya kimataifa. Salehi amesema Harakati ya Nchi Zisizofungamana na Siasa za Upande Wowote ni taasisi kubwa ya kimataifa baada ya Umoja wa Mataifa, yenye uwezo wa kubuni fursa nzuri kwa ajili ya kusogeza mbele malengo ya nchi wanachama wake.
Salehi pia amesisitiza juu ya udharura wa kuanzishwa sekretarieti ya kudumu ya Harakati Nchi Zisizofungamana na Siasa za Upande Wowote na kuongeza kuwa nafasi ya NAM itaimarika kimataifa iwapo kutaundwa sekretarieti ya kudumu kwa ajili ya taasisi hiyo.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameitaja kaulimbiu ya NAM kuwa ni "Uongozi wa Pamoja Kimataifa" na kueleza kuwa wakati umefika sasa kwa uongozi wa dunia kutolewa mikononi mwa baadhi tu ya nchi, na kwamba ili kufikiwa lengo hilo, kuna haja ya kuangaliwa upya muundo wa uongozi duniani.
Viongozi wa karibu nchi 120 wanachama wa NAM watakutana mjini Tehran kuanzia tarehe 26 hadi 31 Agosti.
1055638