IQNA

Al Azhar yawataka Wamisri kizingira ubalozi wa Myanmar mjini Cairo

14:02 - July 19, 2012
Habari ID: 2372536
Kutokana na kushadidi mauaji na ukandamizaji unaofanywa dhidi ya Waislamu nchini Myanmar harakati ya Maulamaa wa al Azhar nchini Misri imetoa taarifa ikitaka kuzingirwa balozi wa nchi hiyo katika maeneo mbalimbali duniani kama ishara ya kulalamikia mauaji hayo.
Harakati ya Maulamaa wa al Azhar imeashiria mauaji, mateso ukatili na vitendo vya kuchomwa moto Waislamu wa Myanmar na vilevile kimya cha nchi za Kiislamu na jamii ya kimataifa mbele ya mauaji hayo na kusisitiza kuwa hii leo suala la kuchomwa moto watoto wadogo limekuwa silaha inayotumiwa na serikali ay Myanmar kwa aliji ya kuangamiza Waislamu.
Shirika la Kutetea Haki za binadamu la Amnesty International limetoa ripoti likisema kuwa askari usalama wa Myanmar wanawatia nguvuni kikatili Waislamu na kubomoa nyumba za maelfu miongoni mwao. Limesema baadhi ya wakimbizi wa Kiislamu waliojaribu kukimbilia Bangladesh kwa kutumia njia ya mto wameghiriki na kufariki dunia.
Rais wa Jamhuri ya Myanmar amesema waziwazi kwamba njia pekee iliyoko mbele ya Waislamu ni kukusanywa katika makambi ya wakimbizi.
Waislamu zaidi ya elfu mbili wameuawa katika siku za hivi karibu nchini Myanmar na wengine zaidi ya elfu 90 wamekimbia makazi yao.
Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiisalmu (OIC) imetoa taarifa ikilaani vikali ukiukaji wa haki za Waislamu nchini humo. 1056061
captcha