IQNA

Ayatullah Nimr asusia chakula kwenye jela

14:42 - July 21, 2012
Habari ID: 2373695
Kituo cha Haki za Binadamu cha Saudia Arabia kimetoa habari ya kuzorota hali ya afya ya Ayatullah Sheikh Nimr Baqir Nimr mwanazuoni na mwanaharakati wa Kishia kutokana na kususia chakula.
Kwa mujibu wa televisheni ya al-Alam kituo hicho cha haki za binadamu kimewanukuu jamaa wa karibu wa mwanazuoni huyo waliomtembelea hospitalini hivi karibuni na kusema kuwa hivi sasa amelezwa katika mojawapo ya hospitali za mji wa Dhahran. Jamaa hao wamesema kwamba baada ya kumtembelea mwanazuoni huyo hospitalini maafisa wa usalama wanaomchunga wamewataka wawaambia watu wanaolalamikia kukamatwa kwake kwamba hali yake ya afya ni nzuri ili kuwatuliza na kuwafanya wasiendelee na maandaamo.
Jamaa hao wamesema kwamba mwanazuoni huyo amepata mateso makali na kwamba hali hiyo inaoonekana wazi usoni na katika meno yake yaliyovunjwa.
Familia ya Ayatullah Nimr inasema kwamba amekuwa akisusia chakula tokea alipokamatwa na kufungwa jela bila kufikishwa mahakamani.
Askari usalama wa Saudia walimtia nguvuni mwanazuoni huyo wa Kiislamu tarehe 8 Julai baada ya kumpiga risasi na kumjeruhi. 1058181
captcha