IQNA

OIC yaanzisha mabadilishano ya wanafunzi katika nchi za Kiislamu

17:33 - July 23, 2012
Habari ID: 2375413
Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC inapanga kuanzisha ‘Mpango wa Mabadilishano ya Kielimu’ katika nchi zote za Kiislamu.
Kwa mujibu wa tovuti ya OIC, mpango huo wa mabadilishano ya wanafunzi hatimye utapelekea kutolewa misaada ya kielimu, masomo kwa njia ya intaneti na miradi ya utafitu katika nchi 57 wanachama.
Mpango huo wa OIC ukikamilika unatazamiwa kuwa mkubwa zaidi wa aina yake duniani.
Mwezi uliopita OIC ilitangaza nafasi 10 za msaada wa masomo (scholarship) katika Chuo Kikuu cha Kuala Lumpur nchini Malayasia.
Uturuki pia imetangaza azma ya kutoa msaada wa masomo katika fremu ya mpango huo wa OIC.
1059979
captcha