IQNA

Chama cha al-Wasat cha Misri chataka balozi wa Myanmar nchini humo asailiwe

13:56 - July 26, 2012
Habari ID: 2377824
Chama cha al- Wasat cha nchini Misri kimetaka balozi wa Myanmar nchini humo asailiwe kuhusiana na mauaji yanayofanywa na serikali ya nchi yake dhidi ya Waislamu wa nchi hiyo.
Chama hicho kinachoongozwa na Abul Ala Madhi kimelaani vikali mauaji hayo ya kinyama yanayofanywa na serikali ya Myanmar na kusisitiza kwamba jambo hilo linakwenda kinyume kabisa na misingi pamoja na sheria za kimataifa zinazosisitiza kuishi pamoja kwa amani wafuasi wa dini tofauti. Katika taarifi aliyotoa hapo siku ya Jumanne, Amr Farouq, msemaji wa chama hicho amemtaka Rais Muhammad Mursi wa Misri kumwita huyo na kumsaili kuhusiana na mauaji hayo ya kinyama yanayoendeshwa kwa mpangilio maalumu na serikali yake. Farouq pia amewataka viongozi wa nchi za Kiislamu kuchukua msimamo thabiti kwa lengo la kutetea na kuwanusuru Waislamu wasio na ulinzi wa Myanmar pamoja na kupeleka faili la mauaji hayo ya kinyama katika Baraza la Usalama. Amesema baraza hilo linapasa kubuni na kutuma kamati ya kutafuta ukweli nchini Myanmar ili kufuatilia kwa karibu suala la kuuawa kikatili Waislamu wa nchi hiyo na pia wahusika kufikishwa mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC. 1062228
captcha