IQNA

Ayatullah Hakim alaani ugaidi wa hivi karibuni nchini Iraq

13:58 - July 26, 2012
Habari ID: 2377825
Ayatullahil Udhma Sayyid Muhammad Said Hakim, mwanazuoni mashuhuri wa Kishia nchini Iraq, amelaani vikali milipuko ya kigaidi iliyotokea siku ya Jumatatu katika pembe tofauti za nchi hiyo.
Amewataka viongoi wa nchi hiyo kuwachukulia hatua kali za kisheria magaidi waliohusika na milipuko hiyo.
Ofisi ya mwanazuoni huyo imetoa taarifa ikisema kuwa damu ya wahanga wa milipuko hiyo haitamwagika bure bali itahifadhiwa katika kitabu kinachohifadhi makubwa na madogo.
Ayatullah Hakim amewataka viongozi wa Iraq kuwa waangalifu na kuchukua hatau za tahadhari kubwa katika kulinda maisha ya wananchi wake.
Tunakumbusha hapa kwamba milipuko hiyo ya kigaidi ya siku ya Jumatatu ilipelekea kuuawa watu 91 na kujeruhiwa wengine wengi. 1062202
captcha