Hayo ni kwa mujibu wa Syed Ali Wasif mtaalamu wa kisiasa mwenye makao yake Washington. Katika mahojiano na Press TV. Wasif ameongeza kuwa Saudi Arabia ni tegemezi kwa nchi za Magharibi na haiwezi kujichukulia maamuzi huru. Amesema sera ya nchi za Magharibi katika Mashariki ya Kati ni kulazimisha Uislamu potofu wa Kiwahabi.
Utawala wa Saudia unaopata himaya ya Marekani umekuwa ukiwakandamiza raia wa nchi hiyo huku wengi wakiuawa na wengine wakisukumwa magerezani katika siku za hivi karibuni.
Wakati huo huo Sambamba na kushadidi malalamiko na maandamano dhidi ya utawala wa Kifalme wa Aali Saud nchini Saudi Arabia katika majuma ya hivi karibuni, gazeti moja la nchini humo limtoa ripoti kuhusu kuongezeka umaskini, ukosefu wa ajira na ufisadi nchini. Imeelezwa kuwa, mambo hayo ni hatari na changamoto kubwa kwa utawala wa nchi hiyo.
Gazeti la Okaz mbali na kuelezea kuvurugika usalama, kulegalega hali ya kisiasa na kuzorota uchumi wa nchi hiyo limeripoti kwamba, Saudi Arabia inajipatia pato la zaidi ya dola bilioni 400 kwa mwaka kutokana na kuuza mafuta ya petroli, lakini licha ya utajiri huo, zaidi ya asilimia 60 ya wananchi wake wanaishi chini ya mstari wa umasikini.
1063363