Vitendo vya ukandamizaji, ubaguzi, mauaji na dhulma wanayofanyiwa Waislamu wa Myanmar imevuka mpaka na kuingia katika jimbo la Assam nchini India.
Jambo hilo limezusha mapigano na mauaji dhidi ya Waislamu wa jimbo hilo na kuwalazimisha wengi wao kukimbia makazi yao kwa ajili ya kutafuta usalama kwingineko.
Kwa mujibu wa tovuti ya On Islam, ghasia hizo zilianza baada ya mwenyeji mmoja wa jimbo hilo kuuawa na watu wasiojulikana. Watu wa kabila la mtu huyo baadaye walishuku na kuwatuhumu Waislamu wa eneo hilo na kuanza kuchoma nyumba zao kiholela kwa kisingizio cha kulipiza kisasi. Kufuatia hujuma hiyo ya kinyama makumi ya Waislamu katika vijiji vilivyolengwa vya Waislamu wameuawa na maelfu ya wengine kukimbia makazi yao.
Katika miaka ya hivi karibuni makabila ya Kihindi na Kikristo ya jimbo lililotajwa yamekuwa yakiwalenga Waislamu wa jimbo hilo kwa vitendo vya kinyama na kigaidi. Asili ya wengi wa Waislamu hao ni Bangladesh.
Kuna Waislamu milioni 160 kati ya jamii ya watu bilioni 1.1 wa India. 1062290