Ayatullah Muhammad Imami Kashani sambamba na kulaani kuuawa Waislamu wa Myanmar na maeneo mengine duniani amesisitiza kwamba, mauaji hayo yameratibiwa na mabeberu wa ulimwengu ili kukabiliana na Uislamu na mwamko wa Kiislamu. Aidha ametahadharisha juu ya njama za maadui wanaopinga mwamko wa Uislamu katika eneo hasa katika nchi za Bahrain na Misri na kuelezea matumaini yake kuwa, mwamko wa Kiislamu na mapinduzi katika nchi za eneo la Mashariki ya Kati yatapata mafanikio kikamilifu. Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya leo hapa mjini Tehran amelaani pia uingiliaji wa mataifa ya kigeni katika masuala ya Syria na kusema kwamba, ana matumaini taifa na serikali ya nchi hiyo itafanikiwa kuyatafutia ufumbuzi matatizo ya hivi sasa kwa kuwa macho na kwa ufahamu.
1063431