IQNA

Iran ni dola lenye nguvu kubwa katika Mashariki ya Kati

8:28 - July 29, 2012
Habari ID: 2379459
Mshauri wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu katika masuala ya kimataifa amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran sasa ni dola lenye nguvu katika eneo la Mashariki ya Kati.
Akizungumza mjini Tehran katika kikao cha qiraa ya Qur'ani cha madaktari wanachama wa jeshi la kujitolea, Basiji, Daktari Ali Akbar Velayati amesema kuibuka Iran kama dola lenye nguvu ni natija ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Ameashiria Mwamko wa Kiislamu katika eneo hili na kusema nchi za Magharibi zinapanga njama za kupotosha mkondo wa mwamko huu.
"Kile ambacho nchi za Magharibi zinajaribu kufanya Syria ni jibu lao baada ya kupoteza ushawishi Iraq, Afghanistan, Misri na Libya."
Dkt. Velayati ambaye aliwahi kuwa waziri wa mambo ya nje wa Iran ameashiria milipuko ya kigaidi wiki iliyopita mjini Damascus na kusema waliopanga hujuma hiyo walikuwa wanataka kuandaa mazingira ya kupitishwa azimio dhidi ya Syria katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Velayati ameongeza kuwa lengo kuu la Wamagharibi katika kuishinikiza Syria ni hatimaye kulenga Iran ambayo sasa imegeuka kuwa dola kubwa lenya nguvu zaidi katika eneo.
1063205
captcha