Kwa mujibu wa gazeti la ar-Rai al-Aam, Idara hizo zimeitaka serikali ya Baghdad kutumia ushawishi wake wote kwa ajili ya kuzitaka pande husika kulinda na kuheshimu maeneo hayo na hasa Haram ya Bibi Zainab (as) dhidi ya hujuma ya makundi ya kigaidi yanayopigana kuangusha serikali halali ya Rais Bashar al-Asad.
Kwa mujibu wa taarifa za idara hizo, pande zote zinazopigana nchini Syria zinapasa kujiepusha na vitendo vyovyote vinavyodhuru na kuharibia heshima maeneo hayo.
Taarifa hiyo pia imezikosoa baadhi ya nchi za Kiarabu zinazochochea na kuyapa silaha makundi ya kigaidi kwa ajili ya kudumisha mapigano haribifu na kuchochea vita vya kikabila na kimadhehebu nchini Syria.
Makundi ya kigaidi yametishia kulipua Haram ya Bibi Zainab mjini Damascus. 1064694