IQNA

Maandamano ya kupinga Aal Saud yafanyika Riyadh, Makka

16:07 - July 30, 2012
Habari ID: 2380977
Maandamano yamefanyika katika miji Mtakatifu wa Makka na huko Riyadh kupinga utawala wa kiimla wa Aal Saud.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, maandamano hayo yamefanyika jana Jumamosi ambapo waandamanaji waliokuwa na hasira wametaka wafungwa wote wa kisiasa waachiliwe huru. Aidha waandamanji wametaka upinduliwe utawala wa kifalme wa ukoo wa Aal Saud ambao unapata himaya ya Marekani.
Ijumaa iliyopita vikosi vya jeshi la Saudia viliwafyatulia risasi waandamanji katika mji wa Qatif mashariki mwa nchi hiyo. Maandamano mengine pia yaliripotiwa katika kijiji cha Awamiya na mji wa Buraydah.
Tokea Februari mwaka 2011, kumekuwepo maandamano katika eneo la Mashariki mwa Saudi Arabia ambapo wananchi wanataka wafungwa wote wa kisiasa waachiliwe huru, uhuru wa maoni na kuhitimishwa ubaguzi. Vikosi vya jeshi la Saudia vimewaua shahidi waandamnaji kadhaa na kuwatia nguvuni wanaharakati wa kisiasa na kidini akiwemo mwanazuoni mashuhuru Sheikh Nemr Nemr.
Wakati huo huo Mkuu mpya wa Shirika la Kijasusi na Usalama la Saudi Arabia ametangaza kuwa, nchi hiyo itahakikisha nchi za Syria, Lebanon na Iraq zinageuka na kuwa kambi za magaidi. Bandar bin Sultan ambaye hivi karibuni alichaguliwa kuliongoza shirika hilo la kijasusi na usalama la nchi hiyo ya Kiarabu, ameyasema hayo alipokutana na Mfalme Abdallah bin Abdul Aziz wa Saudia na kusisitiza kuwa, baada ya kushika wadhifa wa kuliongoza shirika hilo, anakusudia kuziona nchi hizo zilizotajwa zinakuwa ngome za usalama wa mtandao wa kigaidi katika eneo la Mashariki ya Kati.
Hayo yameandikwa na gazeti la Kimarekani la Washington Post na kuongeza kuwa, kiongozi huyo amesema, atahakikisha serikali na bunge la Iraq zinafuata kibubusa siasa za Riyadh.

1064721
captcha